Habari za Kimataifa

RONALDO AWEKA PEMBENI MAMBO YA KOMBE LA DUNIA, ANAKULA BATA KABLA YA KWENDA JUVE

Baada ya kuondolewa kwenye michuano ya Kombe la Dunia alipokuwa nahodha wa Ureno, staa Cristiano Ronaldo ameamua kuweka pembeni masuala ya soka na kuelekeza nguvu zake katika familia.

Ronaldo ametupia picha mitandaoni akiwa na familia yake wakifurahia maisha.

Roanldo 2

Staa huyo kwa sasa anahusishwa kuihama timu yake ya Real Madrid kuelekea Juventus dili ambalo linaonekana lipo hatua za mwisho kukamilika.

Katika picha hizo alizotupia, ameonekana akiwa na mpenzi wake, Goergina Rodriguez, mwanaye Ronaldo Jnr, kaka yake pamoja na watu wengine kadhaa wa familia.