Habari za Kimataifa

CHELSEA WAREJEA MZIGONI, MSIYEMPENDA CONTE YUMKO NDANI! 

Wachezaji wa klabu ya Chelsea wameanza kurejea kwenye mazoezi baada ya kutoka kwenye mapumziko na wengine wakitokea kwenye michuano ya Kombe la Dunia Urusi.

Idadi kubwa ya wachezaji ambao hawakuwemo kwenye michunia ya Kombe la Dunia wamejiunga na mazoezi wakiongozwa na Cesc Fabregas pamoja na David Luiz, Emerson Palmieri na Davide Zappacosta.

Kocha Antonio Conte ambaye anahusishwa kuondolewa klabuni hapo yupo katika mchakato wa kuendelea na kazi yake licha ya kudaiwa kuwa klabu yake imeshawasiliana na kocha mwingine kwa ajili ya kumpa ajira.