Habari za Kimataifa

LOPETEGUI KOCHA MPYA MADRID!

Julen Lopetegui

Real Madrid imetangaza kuwa Julen Lopetegui wa Hispania atakuwa kocha mpya wa klabu hiyo baada ya kumalizika kwa  Kombe la Dunia.

Lopetegui atamfuatia Zinedine Zidane katika kiti cha moto cha Santiago Bernabéu na amesaini mkataba wa miaka mitatu.

 Mchezaji wa zamani wa Los Blancos, mwenye umri wa miaka 51 ambaye amewahi kusimamia timu ya taifa ya Hispania kutoka mwaka 2016, akiwa amewahi kufundisha U19, U20 na U21.

Amewahi pia kuiongoza Rayo Vallecano kwa michezo 11 mwaka 2003, na pia kuifundisha Fc Porto kwa Milka 2 tango mwaka 2014-2016.

 Lopetegui bado hajashinda Kombe lolote katika kiwango cha juu kama meneja, lakini atakuwa na matumaini ya kufanya hivyo katika kombe la Dunia Russia 2018.

 Anakuwa mtu wa 15 wa kuisimamia Real Madrid tangu mwaka 2000.