Habari za Kimataifa

RAIS WA BAYERN MUNICH AINGILIA SAKATA LA USAJILI WA LEWANDOWISKI

lwewandowski44

Wakati dirisha la usajili likiendelea kuwa wazi barani Ulaya, habari ni kuwa Rais wa Klabu ya Bayern Munich, Uli Hoeness amesema hawana mpango wa kumuuza straika wao, Robert Lewandowski.

 Kumekuwa na habari kuwa kwa pauni milioni 176 mshambuliaji huyo ataingizwa sokoni baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka kadhaa tangu alipotokea Borussia Dortmund.

 Uli amesema madai hayo ni ya uwongo na hakuna mpango kama huo wa kumuuza Lewandowiski ambaye ana umri wa miaka 29.

 Manchester United na Chelsea zinatajwa kumuwania huku pia Real Madrid nayo ikihusiswa.