Habari za Kimataifa

DE GEA AULIZWA SWALI LA KUONDOKA MANCHESTER UNITED, APATA KIGUGUMIZI

degea

Ikiwa ni miaka michache imepita tangu kipa David de Gea akwame kwenda Real Madrid katika dakika za mwisho akitokea Manchester United, sakata hilo limekumbushiwa.

 Kwa sasa kipa Hugo anayetajwa kuwa bora duniani yupo katika kikosi cha taifa ya Hispania nchini Urusi kwa ajili ya kushiriki katika Kombe la Dunia.

 Alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu majaaliwa yake, de Gea alisema:

 "Majaaliwa yangu? Kwa sasa muhimu ni kuhusu World Cup, sifikirii kuhusu jambo jingine linaloweza kupoteza mwelekeo wangu.

 "Naeleza nguvu niwe na michuano mizuri, sote tuko vizuri na ninadhani tutafika mbali."