Habari za Kimataifa

BARCELONA YAIPONGEZA MADRID KUCHUKUA UBINGWA UEFA

Barcelona ya Hispania imewapongeza wapinzani wake Real Madrid baada ya kuchukua Kombe la Uefa haps jana kwa kuitandika Liverpool joli 3-1.

Madrid wamechukua Kombe hilo kwa mara ya tatu mfululizo jijini Kiev nchini Ukraine.

 Super Sub Gareth Bale aliifungia Madrid magnolia mawili na kuiandikia historia nyingine ya kuchukua Kombe hilo kwa mara ya 13 .

 Baada ya ushindi huo, Barcelona kupitia ukurasa wake wa Twitter waliandika kuipongeza Madrid kwa ushindi .

Naye nahodha wa zamani wa Barcelona, Carles Puyol aliipongeza Madrid  kupitia mitandao ya kijamii.