Habari za Kimataifa

MANCHESTER UNITED MACHO YOTE KWA DOUGLAS COSTA

dgcosta

MASHETANI wekundu wa Jiji la Manchester, Manchester United, wapo tayari kumsajili winga  Douglas Costa wa FC Bayern Munich anayekipiga kwa mkopo kunako klabu ya Juventus ya Italia.

Taarifa zinaeleza kuwa United wapo tayari kulipa kitita cha £71m, ili kuinasa saini ya Mbrazili huyo iwapo Juventus hawatataka kumnunua moja kwa moja kutoka Bayern Munichen.

douglascosta

Hili litakuwa ni jaribio la pili kwa kocha Jose Mourinho kutaka kumsajili Costa baada ya kujaribu akiwa Chelsea na kuachana na mpango huo kabla staa huyo hajatimkia Bayern Munchen.

Winga huyo mwenye kusifika kwa kasi kubwa, alijiunga na Juventus kwa mkopo msimu uliopita alipopelekwa na aliyekuwa kocha wa Bayern kipindi hicho Carlo Ancelotti kabla hajatupiwa virago kutokanq na matokeo mabaya ndani ya miamba hiyo ya Ujerumani.