Habari za Kimataifa

(VIDEO) KOCHA RAYON SPORTS: NILIJUA YANGA NI WAKUBWA KULIKO SISI

Baada ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika Afrika kati ya Yanga dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda kumalizika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, makocha wa pande zote mbili walizungumza na wanahabari.

Mchezo huo ulimalizika kwa matokeo ya 0-0, ambapo Kocha wa Rayon Sports, Ivan Minnaert ameeleza kuwa kabla ya kucheza mchezo huo pamoja na ule uliopita dhidi ya Gor Mahia alijua kuwa ni timu kubwa kuliko timu yake lakini hiyo haikuwa kigezo cha wao kuziogopa.

“Ndiyo sijafurahishwa na matokeo nafikiri tulicheza vizuri na tulistahili kupata ushindi, tangu mwanzo nilikuwa najua Yanga ni kubwa kuliko sisi, Gor Mahia ni kubwa pia kuliko sisi lakini haimaanishi kuwa kubwa ndiyo tuziogope na leo tumethibitisha kuwa tunaweza kupambana nao,” alisema kocha huyo.