Habari za Kimataifa

EVERTON YATANGAZA KUMTIMUA KAZI KOCHA BIG SAM 

 Kocha Sam Allardyce ametimuliwa katika Klabu ya Everton baada ya kuiongoza timu hiyo kwa muda wa miezi sita tu.

Klabu hiyo ambayo inamiliki Uwanja wa Goodison Park imeshatangaza rasmi juu ya maamuzi hayo ikiwa ni siku chache tangu kumalizika kwa msimu wa 2017/18 katika Premier League.

Awali siku kadhaa zilizopita kulikuwa na taarifa za msigano wa ndani kwa ndani wa kocha na baadhi ya wachezaji huku mashabiki wakisisitiza kuwa kocha huyo anatakiwa kuondoka kwa kushindwa kuisaidia timu kupata mafanikio.

Kocha huyo maarufu kwa jina la Big Sam alichukua nafasi ya Ronald Koeman, Novemba mwaka jana akiikuta timu ipo nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi, hadi ligi inamalizika timu hiyo ilikuwa katika nafasi ya nane.

Kocha huyo anatarajiwa kulipwa pauni 6m kama fidia ya kuvunja mkataba huo.