Habari za Kimataifa

HATIMAYE KIPIGO KWA MAN UNITED CHAIPA UBINGWA MANCHESTER CITY

Kitendo cha Manchester United kukubali kichapo cha bao 1-0 ikiwa nyumbani kutoka kwa West Bromwich Albion kimeifanya timu ya Manchester City kukamilisha mchakato wao wa kubeba ubingwa wa Premier League.

Matokeo hayo yaliyopatikana jana Jumapili yameifanya Man City kuw ana uhakika wa kutofikiwa na timu nyingine yoyote katika Ligi Kuu ya England maarufu kwa jina la Premier League.

 Man United iliruhusu bao hilo katika dakika ya 73 kutoka kwa Jay Rodriguez aliyefunga kwa kichwa baada ya kupigwa kona langoni mwa wenyeji hao.

Matokeo haylo ylipokelewa kwa furaha kubwa na kikosi cha City ambacho kinanolewa na Kocha Pep Guardiola.

Wachezaji kadhaa wa Man City wlaikuwa pamoja kwenye ukumbi wa vinyaji ambapo walishangilia mara baada ya mchezo wa United kumalizika, kisha nahodha wa City, Vincent Kompany akatoa neno la shukrani kwa wenzake waliokuwa wamepagawa kwa furaha.

Kutokana na ubingwa huo, Man City imeingia kwenye orodha ya timu zilizotwaa ubingwa mapema zaidi katika historia ya Premier.

TUJIKUMBUSHE TIMU AMBAZO ZIMEWAHI KUTWAA UBINGWA MAPEMA KATIKA PREMIER LEAGUE

2000-01 Man United (14/04/2001) 

2017-18 Man City (15/04/2018)

1999-00 Man United (22/04/2000) 

2012-13 Man United (22/04/2013)

2003-04 Arsenal (25/04/2004)