Habari za Kimataifa

ARSENAL IMEKATA TAMAA NA PREMIER LEAGUE, YAKUBALI KIPIGO CHA 11

Inavyoonekana ni kama akili ya Arsenal sasa imeelekezwaa zaidi katika michuano ya Europa League, hiyo ni baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 katika Premier League, muda mfupi uliopita.

Arsenal imepata kipigo hicho kutoka kwa Newcastle United katika Ligi Kuu ya England licha ya kuwa yenyewe ndiyo ilianza kutangulia kupata bao kupitia kwa Alexandre Lacazette katika dakika ya 14.

Ikumbukwe kuwa Arsenal ambayo imeshafungwa michezo 11 katika Premier League msimu huu, inajiandaa na mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Europa ambapo itacheza dhidi ya Atletico Madrid.

 Mabao la Newcastle yaliwekwa wavuni na Ayoze Perez dakika ya 29 na Matt Ritchie dakika ya 68