Habari za Kimataifa

MAN CITY WASAFIRI KWENDA UARABUNI KUJIANDAA KUPOKEA TAJI LA PREMIER

Kikosi cha Manchester City ni kama kinaanza maandalizi ya kuupokea ubingwa ambapo kimesafiriki kuelekea Abu Dhabi kwa ajili ya kwueka kambi ya muda.

Man City imeondoka England usiku wa kuamkia leo baada ya ushindi ilioupata wa mabao 2-0 dhidi yua Stoke City katika Premier League.

Ushindi huo unafanya City isubiri mechi mbili tu za kushinda ili ijihakikishie ubingwa wa Ligi Kuu ya England.

Wachezaji wa timu hiyo walionekana wakiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Manchester, saa nane usiku wakipiga picha na baadhi ya mashabiki wachache kabla ya kupanda ndege.

Kiungo wao David Silva ambaye alifunga mabao yote ya jana hajaongozana na wenzake katika safari hiyo kutokana na matatizo ya kifamilia.