Habari za Kimataifa

MANCHESTER UNITED YAPOTEZA MATUMAINI YA UBINGWA, YAPIGWA NA NEWCASTLE UNITED

Manchester United ni kama imeikabidhi Manchester City taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya England ‘Premier League’ baada ya kukubali kichapo cha tano katika msimu huu wa ligi hiyo.

Man United imekubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Newcastle United huku kocha wa United, Jose Mourinho akishindwa kuamini kilichotokea.

Mfungaji wa bao hilo pekee alikuwa ni Matt Ritchie ambaye alifunga katika dakika ya 65.

Kwa matokeo hayo United imebaki nafasi ya pili ikiwa na pointi 56 wakati Man City ipo kileleni ikiwa na pointi 72.