Habari za Kimataifa

VITA YA MAFAHARI WAWILI WA NBA KUAMULIWA FEB. 18

Imeandikwa na Buddah Mtanzania

Kuelekea katika mchezo mkubwa wa Fainali ya Ligi ya kikapu nchini marekani maarufu kama Nba All star utakaochezwa siku ya Tarehe 18 ya mwezi huu wa pili katika Uwanja wa Staples Center, uwanja wa nyumbani wa Klabu ya Los Angels  Lakers kuna vitu vingi vya kutazama ambapo kila mtu atakua anaangalia mchezo huo kwenye televisheni kujua kinachoeendelea nchini Marekani.

Imekua kama desturi kwa michuano hii kuhusisha kanda mbili zenye ushindani katika ligi kuu nchini marekani kwa maana ya ukanda wa mashariki dhidi ya ukanda wa Magharibi ambapo msimu huu imekua tofauti baada ya Michuano hii kuhusisha nyota wawili wenye ushawishi mkubwa katika timu zao. Ukanda wao na ligi kuu ya mpira wa kikapu nchini Marekani(NBA) Stephen Curry akiwakilisha Golden State Warriors na Lebron James akiwakilisha Clevalend Cavarriers.

 Wachezaji hawa wamekua na mvuto katika ligi kuu nchini Marekani kutokana na ubora wao na historia yao katika kuzipatia mafanikio timu zao. Stephen Curry akitwaa tuzo ya Mchezaji bora wa mpira wa kikapu nchini humo(Mvp) mwaka 2014-2015 na kuisaidia timu yake ya Golden State Warriors kutwaa ubingwa wa ligi hiyo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1975 huku akionekana ndiye mchezaji pekee ambaye anaweza kufunga alama tatu katika mtupo mmoja,na kufanya kujizolea umaarufu na Sifa kubwa kwa wapenzi wa mpira wa kikapu hadi kupelekea kupewa jina la Chief Curry kutokana na Ubora wake katika ligi hiyo.

 Lebron James nyota mwenye mafanikio makubwa katika ligi kuu ya kikapu nchini Marekani baada ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya kikapu nchini Marekani(Mvp) kwa mara nne huku akionekana ni mchezaji bora tangu kuondoka kwa nyota kadhaa katika ligi hiyo akiwemo nyota Michael Jordan maarufu kwa jina la Air Jordan,Lebron amekua na mvuto mkubwa katika ligi hiyo na kumfanya kuwa na halaiki kubwa  ya mashabiki kila kona ya Dunia huku akiweka rekodi kadhaa ikiwemo ile ya kufunga Vikapu 30000 katika maisha yake ndani ya ligi hiyo. 

Habari sio Team lebron wala Team Curry ila habari ni namna ambavyo kila mmoja amepewa fursa ya kuchagua wachezaji wake atakaokua nao katika upande wake na kuweza kusaidiana nao kuhakikisha wanapata ushindi katika Fainali hiyo tangu kubadilishwa kwa mfumo wa uchaguaji wa wachezaji kutoka kwenye ukanda hadi kwenye wachezaji wenye mvuto na wanaokubalika(Teams),na kuonekana kuna urafiki na mapenzi katika kuchagua wachezaji Lebron James akimteua Pacha wake wa zamani katika klabu yake Ya Cleveland Cavarries Kyrie Irving ambaye alikua naye katika timu hiyo kwa msimu zaidi ya mmoja hata baada ya kutimkia katika timu ambayo ina historia ya Ubingwa wa Nba ya Boston Celtic.

Wakati Lebron Akimpa nafasi Kyrie Irving mpinzani wake katika fainali hyo Stephen Curry yeye pia ameonesha urafiki wake na mahaba katika uteuzi wa wachezaji akiwateua rafiki zake wa kudumu katika timu yake ya Golden State Warriors Draymond  Green na Klay Thompson ambao walitengeneza muunganiko mzuri katika timu hiyo na kutwaa taji la ligi kuu ya kikapu nchini Marekani msimu uliopita.

Ukiachilia mbali urafiki na mahaba yapo mambo mengi ya kutazama ikiwa ni pamoja na;

Rangi za Jezi 
Baada ya miaka 35 kupita mchezo wa Nba All stars umebadilisha rangi za jezi kutoka katika Rangi nyekundu na Bluu zilizokua zinatumika miaka ya nyuma ambapo ukanda wa Mashariki walikua wakivaa jezi za Rangi ya bluu huku ukanda wa Magharibi walikua wakivaa jezi za rangi nyekundu,tofauti ma hivi sasa ambapo zitatumika Rangi Nyeupe na Nyeusi katika michuano hiyo ambapo timu ya Lebron James itavaa rangi nyeupe wakati team ya Stephen Curry ikivaa Rangi nyeusi.

Vita ya MVP
Hapa ndio kila macho ya mashabiki na wapenzi wa mpira kikapu yalipo kutokana na viwango vya wachezaji mbalimbali  walivyoonesha msimu huu akiwemo nyota wa klabu  ya Houston Rockets ,James Harden aliyevunja rekodi baada ya kufunga vikapu 60 katika mchezo mmoja,Lebron James wa Cleveland Cavaliers,Kyrie Irving  wa Boston Celtic,Russel Westbrook wa Oklahoma City Thunder na Kristap Porzing wa Newyork Knicks ambao wote wamefanya vizuri msimu huu.

Rekodi ya Westbrook na Davis

Wakati wa fainali iliyopita, wachezaji wawili Anthony Davis wa klabu ya New Orlens Pelican na Russel Westbrook wa Oklahoma City Thunder waliweka rekodi ya kuwa wachezaji pekee walioweka rekodi ya kuufanya mchezo wa fainali kua na Jumla ya Vikapu vingi baada ya kila mmoja kufunga vikapu zaidi ya Arobaini na kuweza kuweka mitazamo tofauti juu ya ubora wao na kufanya Russel Westbrook kuwa mchezaji bora kwa maana ya Mvp.

Bifu la Durant na Westbrook

Kabla ya Fainali iliyopita tulishuhudia ugomvi na maneno yaliokua yanatoka midomoni mwa nyota wa Golden State Warriors, Kelvin Durant na Russel Westbrook wa Oklahoma baada ya wawili hao kutengana kutokana na Kelvin Durant kuhama kutoka klabu ya Oklahoma City Thunder na kuhamia Golden State warriors kitendo ambacho kilimuumiza sana Westbrook na kumfanya aseme anamchukia Durant kwasababu hakumwambia kama atahama  katika klabu yake. Msimu huu tutawashuhudia wakiwa katika timu moja ya Lebron James katika fainali hiyo.

Mbali na Fainali hiyo tutashuhudia ushindani mkubwa katika ile Ya kumtafuta Bingwa wa kufunga pointi tatu ambapo Bingwa wa Msimu uliopita Eric Gordon wa Houston Rockets atakua akijaribu kutetea ubingwa wake akichuana na Devin Booker wa Phoenix Suns,Wayne Ellington wa Miami Heat,Paul George wa Oklahoma City Thunder,Bradley Beal wa Washington Wizards,Tobias Harris wa L.A.Clipper na Kyle Lowry wa Toronto Raptors wakati ile michuano ya mitupo ya manjonjo (Slum dunking Contents)itakua ikiongozwa na Aron Gordon ambapo atakua anarejea tena katika michuano hiyo akitafuta ubingwa wake wa kwanza baada ya kutokuwepo kwa mshindi wa michuano iliyopita Glenn Robinson ambaye hajajumuishwa katika mashindano hayo ila ushindani wake upo kwa Denis Smith Jr wa Dallas Mavericks,Victor Oladipo wa Indiana Pacers na mshambuliaji wa Los Angeles Lakers Larry Nance

Vikosi kamili

Team Lebron
Lebron James,Kyrie Irving,Kelvin Durant,Anthony Davis na Paul George,Bradley Beal, Goran Dragic, Victor Oladipo, Kristap Porzing, John Wall na Russel Westbrook

Team Curry
Stephen Curry,James Harden, Demar Derozan, Giannis Antetokoumpo, Joel Emblid, Jimmy Butler,Raymond Greene, Klay Thompson, Kyrie Lowry, Karl Anthony Towns na Damian Lillard.

Tukutane February 18 Los Angeles katika uwanja wa Staples Center hakika itakua ni Fainali yenye Burudani ya Kutosha na Ushindani mkubwa hasa ukilinganisha umaarufu na ubora wa Timu zote Mbili Team Curry  na Team Lebron, Nani ataibuka shujaa kwa upande wake na kuendelea kutengeneza Kambi yake ndani ya Nba na kumfanya kuwa Bora katika upande wa Mashabiki? Tupe maoni yako..