Habari za Kimataifa

HUENDA FLOYD 'MONEY' MAYWEATHER AKARUDI ULINGONI

Ukipitia ukurasa wa Instagram wa Floyd Mayweather, utaona kuna uwezekano wa kurudi ulingoni kupambana. Lakini kurudi huko si katika boxing mchezo ambao umempa heshima na pesa akiwa ameshinda michezo 50 bila kupoteza.

Mayweather ameonekana akijiandaa na mchezo wa Mixed Martial Arts ambao anacheza mpinzani wake aliyepigana naye mchezo wa mwisho kabla ya kutangaza kustaafu Conor MacGregor na wengi wanaamini huenda Mayweather akaamua kurudi ulingoni kupigana na mpinzani wake huyo.

Mayweather hatakua na cha kupoteza akikubali kupambana tena na Mcgregor katika ulingo wa MMA,kwani rekodi ya kushinda au kushindwa katika mchezo huo bado haitaharibu rekodi yake ya boxing aliyonayo zaidi ya kumuingizia mkwanja mrefu.

Conor McGregor naye alipost picha katika mtandao wa instagram baada ya Mayweather kukumbushia kwa picha jinsi alivyompiga Mu Irish huyo mwaka jana.

Mwaka jana rais wa UFC, Dana White alisisitiza kuwa yuko katika mchakato wa kuandaa mpambano wa marudiano kwa mabingwa hao lakini hakuna aliyeamini kwamba mchezo huo utatokea kweli.

Jumanne Mayweather alionekana katika video aliyoposti instagram akiingia katika ulingo unaofanana na ule wanaopigana kina Mcgregor na watu kuanza kuamini kwamba huenda boxer huyo ameanza maandalizi ya mpambano wa marudiano na Conor McGregor. Baada ya video hiyo McGregor Aliandika katika ukurasa wake wa twitter 'Hahahaha,vizuri sana.Endeleza kazi nzuri mwanangu. wako wa dhati, mkubwa.'

 

Mayweather katika ulingo wa MMA akijifua