Habari za Kimataifa

SAFARI YA SANCHEZ KUONDOKA ARSENAL IMEWADIA, ATEMWA KIKOSINI

 

Taarifa za Alexis Sanchez kuondoka ndani ya Arsenal zinazidi kushika kasi hiyo ni baada ya mchezaji huyo kuondolewa katika kikosi kitakachoivaa Bournemouth, leo Jumapili.

Awali Kocha Arsene Wenger alipanga kumtumia Sanchez katika mchezo huo lakini muda mfupi uliopita ilielezwa kuwa mchezaji huyo anayewaniwa na vigogo wawili kutoka Manchester hatakuwemo katika kikosi cha leo.

Sanchez alifanya mazoezi ya oamoja na wenzake jana Jumamosi lakini kuhusu kucheza leo hakusafiri na timu kuelekea katika mchezo huo.