Habari za Kimataifa

ANGELIQUE KERBER AREJEA KATIKA UBORA WAKE

Mcheza tenis namba Moja katika viwango vya mchezo huo mwaka 2016 kwa upande wa wanawake Raia wa Ujerumani Angelique Kerber hii Leo ameshinda taji lake la kwanza

mwaka huu baada ya Hui Leo kumfunga mwanadada Ashleigh Barty katika michuano ya Sydney International kwa Seti 2-0 kwa maana ya (6-4)(6-4) na kufanikiwa kuchukua taji hili.

Mjerumani huyo aliyehangaika sana mwaka uliopita 2017 na kuambulia kua katika nafasi ya 22 katika msimamo wa viwango hivyo kwa upande wa wanawake amesema anajiona mpya 

"Nimecheza kwa kuwashangaza sana watu na najisikia vizuri kushinda taji langu la Kwanza mwaka huu na najisikia kurejea katika nafasi Yang ya kwanza kama ilivyokua Mwaka 2016 "amesema Kerbe.

Sasa Kerber najiandaa kushiriki michuano ya Australian Open(Us open) itakayofanyika huko nchini Australia katika Mji wa Melbone wiki ijayo ambayo atakutana na Nyota kadhaa wa mchezo huo akieemo mwanadada anyeongoza kwa sasa Romania Helep Simo ,Caroline Wozniack wa Denmark anayeshika nafasi ya pili na Mwanadada nwenye uwezo wa hali ya Juu Gabine Muguruza RAIA wa Hispania anayeshika nafasi ya tatu katika ubora na viwango vya mchezo huo kwa upande wa kina mama