Habari za Kimataifa

GOLDEN STATE WAAMKA HUKU CAVS WAKIENDELEA KUSINZIA NBA

Na Buddah Mtanzania

Ligi kuu ya kikapu nchini Marekani imeendelea alfajiri ya Leo huku ikishuhudia Mabingwa watetezi wa michuano hiyo Golden State Warriors wakiamka kutoka kufungwa kwenye mchezo uliopita dhidi ya Los Angeles Clippers leo wamepata ushindi baada ya kufanikiwa kuifunga Milwakee Bucks kwa jumla ya vikapu 108 kwa 94, ambapo nyota wa mchezo wa Leo wakiwa ni Kelvin Durant na Draymond Green wakifunga jumla ya vikapu 47,mirejeo 10 na pasi 3 huku kwa upande wa Bucks wao wameendelea kupata msaada kupitia kwa Gianni's Antetokounmpo aliyefunga vikapu 23 Licha ya timu yake kupoteza katika mchezo huo. Golden State imeendelea kuwakosa Nyota wake wawili Stephen Curry anayesumbuliwa na majeraha ya paja na Klay Thompson ambaye bado Kocha wao Steve Kerry amendelea kumpumzisha.

 

Katika hatua Nyingine washindi wa pili wa msimu uliopita Cleveland Cavaliers wao wamepoteza mchezo wao wa pili mfululizo baada ya kufungwa tena hii Leo na timu ya Indiana Pacers kwa jumla ya vikapu 97 kwa 95 huku ikishuhudiwa Nyota wa Timu hiyo Lebron James akifunga vikapu 27 na pasi 11 wakati Kelvin Love akifunga mirejesho 10 pekee,Huo ni mchezo wapili kupoteza mfululizo baada ya mchezo uliopita kupoteza mbele ya Toronto Raptors ambao msimu huu wanaendelea kufanya vizuri.

 

 

Michezo mingine hii Leo Bradley Beal na John Wall wamefunga jumla ya vikapu 60 na kuiwezesha timu yao ya Washington Wizard kuibuka na ushindi baada ya kuwachapa Orlando Magic vikapu 125 kwa 119. Denver Nuggets wamewafunga Memphis Grizzlies kwa vikapu 87 kwa 78,huku Minnesota Timberwolves wakiwafunga Newyork Knicks vikapu 118 kwa 108,New Orleans Pelican wamewafunga Portland Trair Blazers kwa vikapu 119 dhidi ya 113 ,Atlanta Hawks wamekubali kichapo nyumbani kwa vikapu 105 dhidi ya 110 vya Blooklyn Nets,wakati mchezo wa mwisho Houston Rocket wamewachapa Phoenix Suns vikapu 112 kwa 95 wakiendeleza wimbi la ushindi msimu Huu licha ya kumkosa James Harden aliepata majeraha na sasa kazi kaachiwa Criss Paul aliefunga vikapu 25.