Habari za Kimataifa

KIUNGO WA ARSENAL AKUBALI KUTUA VALENCIA KWA PAUNI 10.5M

Kiungo wa Arsenal, Francis Coquelin amekubali kuhamia Valencia.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 amekuwa mchezaji wa miamba hiyo ya London tangu mwaka 2008 alipojiunga na akademi ya vijana.

Katika misimu ya hivi karibuni, kiungo huyo ameshuka na kukosa namba kikosi cha kwanza akiwa nyuma ya Granit Xhaka, Mohamed Elneny na Jack Wilshere.

Coquelin sasa ameamua kuachana na Arsenal kwa kujiunga na Valencia kwa kiasi kinachokadiriwa kuwa pauni 10.5m.

Klabu nyingine za Uingereza ikiwa ni pamoja na West Ham United, zilitarajiwa kuvutiwa kumsajili Mfaransa huyo.