Habari za Kimataifa

CHELSEA YASHINDWA KUITAMBIA ARSENAL HUKU WENGER AKIWA JUKWAANI

Chelsea na Arsenal zilikuwa na shughuli pevu usiku wa kuamkia leo, katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Carabao Cup 2018 kwenye Stamford Bridge.

 Huo ulikuwa mchezo wa kwanza wa hatua hiyo ambao umemalizika kwa matokeo ya 0-0.

Chelsea ikiongozwa na Kocha Antonio Conte licha ya kuwa nyumbani wameshindwa kupata matokeo ya ushindi dhidi ya Arsenal ambayo ilimkosa kocha wake, Arsene Wenger aliyekuwa jukwaani.

Wenger alikuwa jukwaani kutokana na kufungiwa kutokukaa katika benchi katika mechi tatu.

Kwa matokeo hayo sasa Chelsea atakuwa na mtihani mzito katika mchezo wa marudiano ambao utachezwa kwenye Uwanja wa Emirates ambao ni dimba la nyumbani la Arsenal.