Habari za Kimataifa

OKLAHOMA CITY THUNDER YAENDELEA KUTOKOTA NBA

 

Timu ya soka ya mpira wa kikapu ya nchini Marekani Oklahoma City Thunder, alfajiri ya leo wamepoteza mchezo wao katika muendelezo wa ligi kuu ya kikapu nchini Marekani  baada ya kufungwa na timu ya Portland Trail Blazers kwa vikapu 117-106.

Katika mchezo huo umeshuhudia nyota wa Oklahoma City Thunder, Russell Westbrook ameshindwa kuendeleza rekodi yake ya kufunga Triple Double baada ya kufunga vikapu 22, mirejesho 9 na pasi 12 akiwa amekosa mrejesho mmoja kufikisha Triple Double ya 15 msimu huu.

Ikumbukwe msimu uliopita Westbrook alivunja rekodi ya mkongwe Oscar Robertson aliyoiweka mwaka 1962 kwa kufunga triple Double 42 huku westbrook akifunga zaidi ya 50

Katika hatua nyingine wachezaji Serge Ibaka na James Johnson walitolewa nje kwenye mchezo wa timu zao za Miami Heat dhidi ya Toronto Raptors baada ya kupigana uwanjani kutokana na kutupiana maneno hali iliyosababisha mwamuzi wa mchezo huo kuwatoa nje katika mchezo ambao Miami Heat wameifunga Toronto Raptors kwa vikapu 90 dhidi ya 89 vya Raptors.

Pia ilishuhudiwa nyota wake, Kyle Lowry akipata majeraha na kushindwa kuendelea na mchezo baada ya kutolewa nje katika robo ya tatu katika mchezo huo uliochapwa  katika dimba la Air Canada Center nchini Canada matokeo mengine wafalme wa Sacramento {Sacramento Kings} wakipoteza nyumbani dhidi ya Los Angeles Lakers kwa vikapu 86-99 huku Orlando Magic wakipoteza dhidi ya Dallas Mavericks kwa vikapu 99-114.

Ligi hiyo itaendelea kwa kuzikutanisha timu zenye kushika nafasi za juu katika ukanda wa Eastern Conference, Cleveland Cavaliers inayoshika nafasi ya tatu dhidi ya Toronto Raptors inayoshika nafasi ya pili katika ukanda huo ambao hadi sasa unaongozwa na mabingwa wa kihistoria wa ligi hiyo, Boston Celtic.