Habari za Kimataifa

STEPHEN CURRY AREJEA KWA KISHINDO, AIPA TIMU YAKE USHINDI NBA

Baada ya kusumbuliwa kwa majeruhi muda mrefu na kusababisha kukosekana katika timu yake kwenye michezo mitano, nyota wa timu ya kikapu katika Ligi ya NBA ya Marekani, Stephen Curry

ambaye anaichezea Golden State Warriors amerejea na kuipa ushindi timu yake katika mchezo mgumu alfajiri ya leo dhidi ya Houston Rockets kwa vikapu 124-114.

Katika mchezo huo, Curry amefunga pointi 29, mirejeo 9 na asisti 5, huku nyota mwenzake wa timu hiyo Draymond Green akipata Triple Double katika mchezo huo kwa kufunga vikapu 17 mirejesho 14 na asisti 10 na kuifanya timu yao kubuka na ushindi.

Upande wao Rocket wao walikuwa wakimtegemea nyota wao ambaye ni mshindi wa michuano ya Slum Dunk, Erick Gordon baada ya kuumia kwa nyota wao, James Harden, katika mchezo huo, Gordon amefunga vikapu 30 na pasi 7 huku mchezaji mwenzake Green akifunga vikapu 29 lakini havikutosha kuipatia ushindi timu yake ya Rocket.

Wakati huohuo, nyota wa Oklahoma City Thunder, Russel Westbrook ameendelea kuweka rekodi ya kufunga triple double katika michuano hiyo baada ya alfajiri ya leo kufunga vikapu 29 mirejeo 12 na pasi 11 na kuisaidia timu yake kupata ushindi dhidi ya timu ya Los Angeles Clippers kwa ushindi wa vikapu 127-117 huku akipewa ushirikiano wa karibu na mchezaji mpya katika timu hiyo aliyetokea Indiana Pacers mtaalamu Paul George aliyefunga vikapu 31 pasi 3 na mirejeo 6.

Clippers wao nyota wa mchezo kwa upande wao katika mchezo wa leo alikuwa ni Lou Williams na Danny Jordan waliofunga jumla ya vikapu 52.

Wakati huohuo, kura za kumtafuta mchezaji bora katika mwaka huu 2018 zimeanza kupigwa na nyota wa timu ya Milwaukee Bucks na timu ya taifa ya Ugiriki mwenye umri wa miaka 22, Giannis Attequmpo ameweka historia kwa kumshinda Mfalme wa NBA kwa sasa, Lebron James wa Cleveland Cavaliers katika kura hizo.

 

Raundi ya kwanza ya kura hizo ipo hivi….

Giannis Attequmpo - 863,416

LeBron James - 856,080

Kyrie Irving - 802,834

Kelvin Durant -767,402

Steph Curry - 735,115

James Harden - 602,040