Habari za Kimataifa

MICHUANO YA SOKA LA UFUKWENI (COPA DAR ES SALAAM) KUANZA LEO

Soka la ufukweni lianzidi kushika kasi nchini Tanzania, hiyo ni kutokana na mwendelezo wa michuano mbalimbali inayofanyika nchini Tanzania. 

Mashindano ya Copa Dar es Salaam yanatarajiwa kuanza leo Desemba 25 na yataendelea hadi kesho Desemba 26 kwenye Ufukwe wa Coco.

Tayari timu zimeshawasili na zitakazoshiriki ni timu za Malawi, Zanzibar wenyeji Tanzania Bara na Uganda.

Yanga haijataka kufanya makosa kama ambavyo wapinzani wao wa jadi, Simba walifanya juzi katika michuano ya Kombe la FA.

Yanga imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Reha FC kwenye mchezo wa Azam Sports Federation Cup (ASFC) maarufu kwa jina la Kombe la FA, jioni ya leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Waliocheka na nyavu ni kiungo Pius Buswita na mshambuliaji Amissi Tambwe na hivyo kusonga mbele katika hatua ya 32 Bora ya michuano hiyo.

Mchezo huo ulikuwa mzuri kwa Tambwe ambaye alikuwa majeruhi kwa muda mrefu, kurejea kwake kumuekuwa na neema kwa Wanayanga hasa kutokana na safu yao ya ushambuliaji kuonekana kupunguza makali.