Habari za Kimataifa

REAL MADRID YAPOKEA KICHAPO NYUMBANI,MESSI SUAREZ WAPELEKA KILIO

Klabu ya FC Barcelona imeibuka na ushindi kwa kuifunga Real Madrid kwa mabao 3-0 katika El Clasico mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu jijini Madrid, Mechi hiyo ilikuwa tamu na ya kuvutia na hadi mapumiziko hakukuwa na mbabe aliyegusa nyavu za mwenzake.

Kipindi cha pili kilikuwa kichungu kwa Madrid ambayo ilikubali mabao mawili ya Luis Suarez na Lionel Messi aliyefunga kwa mkwaju wa penalti huku Madrid ikicheza pungufu baada yabeki wake wa kulia, Dani Carvajal kulambwa kadi nyekundu baada ya kuunawa mpira makusudi akiuzuia usitinge wavuni

Madrid walipata zaidi ya nafasi tatu za kufunga katika kipindi cha kwanza, lakini mabingwa hao wa dunia mara mbili mfululizo, walishindwa kufunga kupitia Cristiano Ronaldo na Karim Benzema.