Habari za Kimataifa

MTIFUANO WA EL CLASICO LEO DUNIA YOTE ITASIMAMA

 

Real Madrid inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Barcelona katika mchezo wa La Liga ambapo timu hizo zinapokutana mchezo huo unajulikana kwa jina la El Clasico.

Madrid imepanga leo kuonyesha kombe ililotwaa kabla ya mchezo dhidi ya Barcelona kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu.

"Tunaweza kutoa heshima hiyo endapo ingekuwa tunazungumzia Ligi ya Mabingwa Ulaya au La Liga, lakini siyo kwa ubingwa huu," alisema Mkurugenzi wa Barcelona, Guillermo Amor.

Upande wa staa wa Barcelona Lionel Messi atakuwa na nafasi nyingine ya kuendeleza rekodi yake ya kufunga mabao mengi katika El Clasico kwani katika mabao 24 aliyofunga 14 ameyafunga nyumbani kwa Madrid.

Messi alianza kuifunga Madrid mnamo Mei 2, 2009 akiwa chini ya Kocha Pep Guardiola ambapo alifunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 6-2 ambao bado unakumbukwa.

Hadi sasa katika La Liga, Messi anaongoza kwa ufungaji akiwa na mabao 14 msimu huu katika La Liga, hivyo ana nafasi ya kujiongezea mabao katika mchezo wa leo.