Habari za Kimataifa

VIGOGO KUTIFUANA LIGI YA MABINGWA ULAYA, MAN U INAWEZA KUIVAA REAL MADRID

Baada ya matokeo ya mechi za jana usiku katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, sasa mambo yanaelekea kuwa matamu ambapo, timu zitakazocheza hatua ya mtoano ya michuano hiyo zimeshajulikana.

Michuano hiyo ambayo itaendelea Februari mwakani itazikutanisha timu vigogo kwa kuwa zile zilizoshika nafasi ya kwanza katika hatua ya makundi zitakipiga dhidi ya zile zilizoshika nafasi ya pili

Timu ambazo zipo katika hatua ya kupangwa kukutana kwenye hatua inayofuata zipo katika makundi mawili, zile zilizoshika nafasi ya kwanza na nafasi ya pili katika hatua ya makundi, Real Madrid inaweza kukutana na yoyote kati ya walioshika nafasi ya kwanza ikiwemo Man United:

WALIOSHIKA NO 1

Manchester United

Paris Saint-Germain

Roma

Barcelona

Liverpool

Manchester City

Beşiktaş

Tottenham Hotspur

 

WALIOSHIKA NO 2

Basel

Bayern Munich

Chelsea

Juventus

Sevilla

Shakhtar Donetsk

Porto

Real Madrid