Habari za Kimataifa

KUELEKEA MANCHESTER DERBY, MOURINHO AMRUSHIA DONGO GURDIOLA, AMJUMUISHA NA WENGER

 

Mchezo wa Manchester United dhidi ya Manchester City unaojilikana kwa jina la Manchester Derby, unatarajiwa kupigwa wikiendi hii ambapo tayari mambo yameanza kunoga. 

Kama kawaida Jose Mourinho wa Man United na Pep Guardiola wa Man City mara zote wamekuwa wakitupiana vijembe, tayari Mourinho ameanza maneno kwa kumshutumu Guardiola kwamba anadanganya kuhusu majeruhi.

Guardiola alinukuliwa akisema kwamba David Silva ni majeruhi na anaweza kukosa mchezo wa derby, jambo hilo limepokelewa tofauti na Mourinho kwani anaamini siyo kweli na Pep anajua kwamba Silva atakuwepo.

Mourinho amedai kwamba yeye kwa upande wake hawezi kusema uongo hata siku moja kuhusu majeruhi, na majeruhi wote ambao Mourinho alisema awali hawatakuwepo katika kikosi hicho hawatakuwepo kweli.

United wanakutana na City ambao msimu huu wanaonekana kuwa tishia kubwa si tu nchini England bali barani Ulaya kwa jumla, kama City atashinda mchezo huu atazidi ongeza pengo la alama kati yake na United na United wanahitaji kushinda ili kupunguza pengo.