Habari za Kimataifa

PICHA: HIVI NDIVYO MSUVA, SINGANO WALIVYOANZA KAZI PAMOJA MOROCCO

 Winga wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, Simon Msuva aliyekuwa anaichezea Yanga, Jumapili ya juzi ikiwa ni siku nne zimepita toka asaini mkataba na timu ya Difaa El Jadid ya Morocco, alianza kucheza mwechi pamoja na wenzake.

Msubva alipata nafasi ya kuichezea Jadid mchezo wa kwanza wa kirafiki na kufunga bao licha ya timu yake kupoteza kwa mabao 2-1.

Kocha wa Jadid aliamua kuchezesha vikosi viwili katika mchezo huo ambapo kila kikosi kilicheza kwa dakika 45.

Dakika 45 za kwanza kocha wa El Jadid alichezesha wachezaji aliyopandisha kutoka team B na wachezaji wanaofanya majaribio ambapo kikosi hicho kilifungwa magoli mawili na ndiyo dakika 45 za pili Simon Msuva na wachezaji wengine wakaingia.

Katika mchezo huo pia, Ramadhani Singano ambaye naye ni Mtanzania alipata nafasi ya kucheza katika kikosi hicho akiwa pamoja na Msuva. 

Singano ametua klabuni hapo akitokea Azam FC wakati Msuva ametokea Yanga.