Habari za Kimataifa

Timu ya Manchester United imetinga fainali ya michuano ya Europa League licha ya kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Celta Vigo, usiku wa kuamkia leo.

Man United sasa itacheza dhidi ya Ajax Amsterdam ya Uholanzi ambayo imeitoa Lyon ya Ufaransa,

Fainali ya michuano hiyo itachezwa Mei 24, mwaka huu jijini Stockholm nchini Sweden.

Katika mchezo huo wa nusu fainali dhidi ya Celta Vigo ya Hispania ambayo iliing’oa KRC Genk anayochezea Mtanzania Mbwana Samatta katika hatua ya robo fainali, ushindani ulikuwa mkali na hata Kocha wa Man United, Jose Mourinho alikiri mambo yalikuwa magumu.

Shujaa wa Man United alikuwa Marouane Fellain aliyefunga bao la mapema kwa kichwa kabla ya Vigo kusawazisha na kufanya United kusonga mbele kwa jumla ya mabao 2-1

Fellain akifunga goli.

Refa wa mchezo aliwatoa BAILY wa manchester united pamoja na RONCAGLIA wa celta vigo baada ya kufanyiana vurugu.

 

Baraza la Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limeidhinisha mpango wa kulipatia Bara la Afrika nafasi 9 wakati Kombe la Dunia litakapoongeza timu zitakazoshiriki katika kinyang'anyiro hicho na kufikia 48, 2026.

Hatua hiyo ilithibitishwa siku ya Jumanne mjini Bahrain. Kwa sasa bara hilo lina nafasi 5 pekee.

Taifa la kumi la Afrika litashiriki katika mchuano wa muondoano utakaojumuisha mataifa sita ili kuamua kuhusu nafasi mbili.

Baraza la Fifa lilipendekeza vile litakavyotoa nafasi hizo 48 mnamo tarehe 30 mwezi Machi. kinyang'anyiro hicho kipya kitashirikisha timu 16 kutoka Ulaya.

Wanachama wa Fifa walipiga kura mnamo mwezi Januari kuongeza timu zitakazoshiriki kutoka 32 hadi 48 kuanzia dimba la mwaka 2026