HASSAN KESSY:ATAJA KILICHOWAFANYA YANGA KUIBUKA NA USHINDI

by Harun, 4 months ago
0

bao la dakika ya 90 la beki Hassan Ramadhani Kessy limeipa ushindi wa 1-0 Yanga SC dhidi ya JKU katika mchezo wa Kundi B Kombe la Mapinduzi jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.Sifa zimuendee mwenyewe Kessy kwa bao hilo, kwani aliingia na mpira ndani kwa kasi kutokea pembeni akampasia Pius Buswita aliyemsogezea mbele beki huyo kwa pasi ya kisigino akaikuta na kufunga.Kwa ushindi huo mwembamba, Yanga SC inafikisha pointi sita baada ya mechi mbili, ikiwemo ya kwanza waliyoshinda 2-1 dhidi ya Mlandege juzi.