YANGA 2-1 MLANDEGE :MFUNGAJI MAGOLI YOTE JUMA MAHADHI |MAPINDUZI CUP

by Harun, 4 months ago
0

Yanga imefanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mlandege katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi uliochezwa ndani ya Uwanja wa Amaani kisiwani Zanzibar.Mabao ya Yanga katika mchezo huyo yote yamefungwa na kiungo mshambuliaji Juma Mahadhi wakati lile la wenyeji Mlandege liliwekwa wavuni na Makame.Mchezo huo ambao ulikuwa wa kwanza kwa Yanga ulimalizika kwa wachezaji wa pande zote mbili kupewa kadi nyekundu, ambao ni Makame wa Mlandege na beki wa kati wa Yanga, Dante ambaye jina lake halisi ni Andrew Vincent, sababu ikiwa ni wachezaji hao kuonyeshana ubabe uwanjani katika kipindi cha pili.