BEKI MTATA:Aingizwa kikosini simba kuwavaa Al masry

by Harun, 4 months ago
0

Wakati Simba ikiwa safarini kutoka Tanzania kuelekea nchini Misri kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Al Masry, kuna mabadiliko ya kiufundi yamefanyika.Simba itakuwa nchini humo kukipiga katika mchezo wa pili wa Kombe la Shirikisho ambapo katika mchezo wa kwanza ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2.Kocha Mkuu wa Simba, Pierre Lechantre ambaye ni raia wa Ufaransa ameweka wazi kuwa mipango yao ni kumrejesha katika kikosi cha kwanza beki wao wa kati, Juuko Murshidi raia wa Uganda.Juuko ambaye kwa muda mrefu amekuwa hachezi kikosi cha kwanza cha Simba, Jumamosi ijayo anatarajiwa kuwa sehemu ya wachezaji wa kikosi cha kwanza cha timu hiyo kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa kwenye Uwanja wa Port Said, Misri.Mchezo huo utakaochezeshwa na mwamuzi wa kati Yonas Zekarias Ghebre akiwa na wasaidizi wake wote wakiwa ni raia wa Eritrea, unatarajiwa kuwa mkali kwa kuwa timu zote bado zina nafasi ya kusonga mbele.Maamuzi hayo yalifikiwa katika mazoezi yao ya mwisho kabla ya timu hiyo kusafiri kuelekea Misri, ambapo Lechantre aliamua kumpa Juuko majukumu maalum ya kuhakikisha anasaidiana na wenzake katika kukabiliana na washambuliaji wa Al Masry.Kwenye mazoezi yao hayo yaliyokuwa yakifanyika kwenye Uwanja wa Boko jijini Dar, Lechantre alipanga kikosi ambacho kinaonekana ndicho kinaweza kuanza Jumamosi ambapo pia Juuko yupo.Kikosi hicho kilikuwa hivi; Aishi Manula, Nicholaus Gyan, Asante Kwasi, Erasto Nyoni, Juuko Murshid, James Kotei, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Shomary Kapombe, Emmanuel Okwi na Laudit Mavugo.Upande wa mshambuliaji John Bocco alikuwa akitumia muda mwingi kufanya mazoezi maalum ya peke yake kwa kuwa aliumia katika mchezo uliopita dhidi ya Waarabu hao.Juuko raia wa Uganda anajulikana kwa kucheza soka la nguvu na mara nyingine la kibabe ambapo amekuwa akipata kadi mara kadhaa kutokana na staili yake hiyo.Hata katika mchezo uliopita Simba walimtumia Yusuf Mlipili katika nafasi ya ulinzi wa kati, dalili zinaonyesha kutakuwa na mabadiliko katika mchezo wa marudio.