KAMUSOKO, AJIBU, Walivyoshuka Taifa kuwavaa Stand United

by Guest, 3 months ago
0

Yanga wanatarajiwa kushuka uwanjani leo Jumatatu katika kipute cha Ligi Kuu ya Vodacom kukipiga dhidi ya Stand United.Beki wa kulia wa Yanga, Juma Abdul amesema kwamba ni muhimu mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani, kwani hiyo itawapa hamasa wapigane na kushinda leo.Upande wa kipa chipukizi Kabwili yeye amesema kwamba mashabiki wa Yanga hawapaswi kujiweka nyuma, wanatakiwa kujitokeza kwa wingi uwanjani kuwapa sapoti wachezaji wao na akasema wao watapigana washinde mchezo wa leo. Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Juma Mahadhi amesema kwamba ushindi leo ni muhimu na zaidi malengo yao ni ubingwa wa Ligi Kuu, hivyo amewaomba wapenzi wa Yanga wajitokeze uwanjani kwa wingi leo.