WALICHOKISEMA AZAM KUHUSU OKWI NA JONAS MKUDE

by Harun, 5 months ago
0

SIMBA SC imezidi kuwaacha mbali wapinzani katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Hongera kwake mfungaji wa bao pekee la leo, mshambuliaji Mganda Emmanuel Arnold Okwi aliyefunga dakika ya 36 baada ya kutokea patashika kwenye lango la Azam FC kufuatia krosi ya beki Mghana, Asante Kwasi.Simba SC sasa inafikisha pointi 41 baada ya kucheza mechi 17, wakiwazidi kwa pointi saba, mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 34 katika nafasi ya pili na Azam FC wanabaki nafasi ya tatu kwa pointi zao 33