Magoli Lipuli 1 - 1 Simba

by Harun, 2 months ago
0

WEKUNDU wa Msimbazi Simba SC, leo hii wamevutwa shati na Lipuli FC, katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Samora mjini Iringa.Ilichukua dakika takribani 31 kwa Lipuli kuweza kuandika bao la utangulizi kupitia kwa mshambuliaji wao Adam Salamba, aliyeipangua vyemq ngome ya ulinzi ya Simba na kupiga shuti kali lililomshinda Aishi Manula na kutinga katika nyavu huku ubao ukisomeka Lipuli 1_0 Simba hadi kipindi cha kwanza kinakwisha.Benchi la ufundi la Simba lilifanya mabadiliko kwa kumtoa mlinzi Juuko Murdhid na kumuingiza Laudit Mavugo katika dakika ya 46 ya mchezo mabadiliko yaliyoonekana kuwa na manufaa kwa vinara hao wa Ligi kuu Bara.Mnamo dakika ya 66 ya mchezo, Mavugo aliweza kusawazisha bao hilo kwa kumalizia kona safi iliyochongwa na Shomari Kapombe na kufanya ubao kubadilika na kusomeka mabao 2_2 hadi mwisho wa mchezo.Huu umekuwa mchezo wa pili kwa Simba kulazimishwa sare ya bao 1_1 na Lipuli, kufuatia mchezo wa kwanza iliochezwa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, kumalizika kwa matokeo kama hayo huku magoli yakifungwa na Mwinyi Kazimoto kwa upande wa Simba na Asante Kwasi kwa ukiwasawazishia Lipuli kwa faulu mwanana iliyomshinda mlinda mlango wa Simba Aishi Manula na kujaa kimiani.Simba sasa wataziekeza nguvu zao zote katika mchezo unaofuata April 29 dhidi ya watani wao wa jadi Yanga, mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.