Simba 3 -1 Mbeya City | Magoli

by Harun, 2 months ago
0

Simba Sc imeongeza kasi kulikimbilia taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni ya leo.Ushindi huo unawafanya Wekundu hao wa Msimbazi wafikishe pointi 55 baada ya kucheza mechi 23, moja zaidi ya mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 47 katika nafasi ya pili.Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Hance Mabena wa Tanga aliyesaidiwa na Jesse Erasmo wa Morogoro na Rashid Zongo wa Iringa, hadi mapumziko Simba SC walikuwa tayari wamekwishavuna ushindi huo wa mabao 3-1.