Magoli Yanga 1 -1 Singida United

by Harun, 3 months ago
0

MATUMAINI ya Yanga SC kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara yameanza kutoweka taratibu baada ya leo kulazimisha sare ya 1-1 na Singida United Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.Sare hiyo inaiongezea Yanga pointi moja tu na kufikisha 47 baada ya kucheza mechi 22, ikizidiwa pointi tano na vinara, Simba SC wenye pointi 52 za mechi 22 pia. Katika mchezo wa leo uliochezeshwa na refa Jacob Adongo wa Mara aliyesaidiwa na Ferdinand Chacha wa Mwanza na Janeth Balama wa Iringa