TAZAMA:Magoli yote ya yanga 2 - 0 Welayta Dicha

by Harun, 3 months ago
0

TIMU Yanga leo imetoka kifua mbele baada ya kuitandika timu ya Wolaitta Dicha kutoka Ethiopia magoli mawili bila.Goli la mapema la yanga lilipatikana kwenye dakika ya kwanza ya mchezo kupitia kwa Raphael Daudi baada ya kuunganisha krosi safi iliyopigwa na Ibrahim Ajibu,Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza kinamalizika Yanga walikuwa mbele kwa goli moja bila.Goli la pili la Yanga lilipatikana kupitia kwa Emanuel Martin kwenye kipindi cha pili matoke ambao yalidumu mpaka mwisho wa mpira.Timu hizi mbili zitakutana baada ya wiki moja ijayo kwa ajili ya mchezo wa marudioano