KOCHA WA URA: NAIOGOPA YANGA

by Harun, 6 months ago
0

Michuano ya Kombe la Mapinduzi inaendelea kisiwani Zanzibar na tayari imefikia hatua ya nusu fainali, Yanga imepangwa kucheza dhidi ya URA ya Uganda wakati Azam FC itapepetana na Singida United.Wakati hatua hiyo ikifikiwa, siku chache kabla, Kocha wa URA, Nkata Paul alinukuliwa akisema kama timu yake itafanikiwa kusonga mbele kwenye michuano hiyo basi hapendi kukutana na Yanga.Hivyo ka kauli hiyo huku timu hizo zikiwa zimeshapangwa kukutana inaonyesha wazi kuwa kazi ipo. Nusu fainali hizo zitacheza Jumatano ya Januari 10 kwenye Uwanja wa Amaan.Nkata alinukuliwa akisema Yanga ndiyo timu ambayo anaihofia kukutana nayo kutokana na mfumo wanaotumia na wachezaji waliokuwa nao ambao siyo rahisi kuwadhibiti kutokana na kubadilika mara kwa mara.Akifafanua zaidi kocha huyo alisema hivi: "Kitu kinachonifanya kuihofia Yanga kwanza ni timu ambayo huwezi kuikariri kila siku inakuja na kikosi kipya na wachezaji wake wengi ni vijana, wana kasi na nguvu za kupambana ukilinganisha na timu nyingine hicho ndiyo kina nifanya niwe na hofu ya kukutana nao," alisema Nkata.Kocha huyo amesema anatambua kwamba Yanga inawakosa baadhi ya wachezaji wake wenye uzoefu na majina makubwa lakini vijana waliopo kwake yeye ndiyo anaona ni hatari kuliko wachezaji hao ambao wangeifanya timu kutokuwa na tofauti na Simba na Azam FC.Pamoja na yote kocha huyo alisema kama itatoke wakakutana na Yanga basi atalazimika kubadili mfumo wa uchezaji kwa timu yake na kutumia sana uzoefu wao ili kuweza kushinda mchezo huo na kutinga fainali kwa mara nyingine kama walivyofanya mwaka juzi ambapo waliifunga Yanga kwa mikwaju ya penalti na kucheza fainali na Mtibwa Sugar.