TAZAMA SIMBA VS JAMHURI | MAGOLI KIPINDI CHA KWANZA

by Harun, 4 months ago
0

Simba imeamka katika michuano ya Mapinduzi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Jamhuri ya Pemba.Mabao ya Simba, yamefungwa na John Bocco, Moses Kitandu na beki mpya wa Simba, Asante Kwasi.Simba ilionyesha kiwango kizuri katika mechi hiyo baada ya kuwa imeanza kwa sare katika mechi ya kwanza dhidi ya Mwenge.Kiungo wake, Gyan Asamoh raia wa Ghana naye alicheza vizuri katika mechi hiyo na kutoa pasi ya bao la pili lililofungwa na Kitandu, mkongwe Mwinyi Kazimoto akatengeneza bao la Bocco huku Bocco akimtengea Kwasi aliyefunga kwa kichwa.