LWANDAMINA ANACHOWAZA NI KUISHUSHA SIMBA TU

by Harun, 7 months ago
0

Pamoja na kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo lakini kocha wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom, Yanga, George Lwandamina ametamba kuziondoa Simba, Azam FC juu kwenye usukani wa ligi hiyo. Lwandamina amesema mazoezi wanayofanya hivi sasa yanalengo la kuhakikisha wanarudi kileleni na kutwaa ubingwa kama walivyofanya misimu mitatu iliyopita. Kocha huyo raia wa Zambia amesema anatambua kuwa kila shabiki na mwanachama wa timu hiyo anahitaji kuona Yanga inatwaa ubingwa na yeye atahakikisha hilo linatimia kwa kutokana na ari pamoja na maandalizi wanayoyafanya kwenye mazoezi yao. "Tunafanya mazoezi kwa malengo dhamira yetu ni kutetea ubingwa na hilo linawezekana kutokana utayari tuliokuwa nao najua ugumu uliopo kwenye ligi ya msimu huu lakini hilo haliwezi kutuzuia kwani msimu uliopita yalikuwepo hayo lakini bado tupo imara na tunaendelea na mapambano," alisema Lwandamina.